Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya Choo Duniani: Tumia ubunifu kwa usafi na mazingira salama

Fermín alikuwa mtu wa kwanza katika jumuiya yake kutengeneza choo, kutokana na kampeni ya UNICEF Colombia na Wakfu wa Kimataifa wa Baxter.
© UNICEF/Colombia
Fermín alikuwa mtu wa kwanza katika jumuiya yake kutengeneza choo, kutokana na kampeni ya UNICEF Colombia na Wakfu wa Kimataifa wa Baxter.

Siku ya Choo Duniani: Tumia ubunifu kwa usafi na mazingira salama

Tabianchi na mazingira

Ubunifu umeenea katika mbio za kupanua upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira duniani kote wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Choo Duniani, hii leo tarehe 19 Novemba.

Sambamba na kaulimbiu ya mwaka huu ya kuongeza kasi ya mabadiliko, wavumbuzi wamekuwa sehemu ya juhudi zinazoendelea kushughulikia mahitaji ya takriban watu bilioni 3.5 duniani wanaoishi bila vyoo salama.

Kutoka kwa mwanamke wa Kinepali ambaye alichochea kijiji chake kuboresha usafi hadi mpango mpya wa mchezo uliozinduliwa mwaka wa 2022 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, wabadilishaji mchezo hawa wanasonga mbele kuelekea azma ya Ajenda ya 2030 ya kufikia maji safi na usafi wa mazingira kwa wote kupitia Mpango wake wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG lengo la sita (SDG) 6.

Na ndivyo ilivyo kwa kundi la vijana wanaoendesha uvumbuzi wa usafi wa mazingira huko Kisumu, Kenya.

Choo kilichoshinda tuzo

Saniwise Technologies, kampuni inayoundwa na timu ya vijana wajasiriamali vijana, ilibuni choo kinachojali kutunza mazingira ambacho kilishinda tuzo ambacho pia kinazalisha samadi na chakula cha kuku.

“Baada ya kulelewa pekee na mama katika eneo la watu wa kipato cha chini, ninaelewa changamoto,” alisema Chelsea Johannes kutoka kampuni ya Saniwise. “Ni vigumu kutunza vyoo, na hakuna anayetaka kuchangia pesa ili kuvizibua ipasavyo. Hiyo ndiyo sababu moja ya sisi kuanzisha Saniwise.”

Kwa kutumia mitambo yake ya buluu, yenye uingizaji hewa wa kutosha, timu ya Saniwise inalenga kutengeneza vyoo vingi zaidi kwa ajili ya jamii, alisema.

Tayari imeshinda pesa za kuanza kufanya hivyo, baada ya mfano wake wa choo kutwaa tuzo ya pili katika shindano la kimataifa lililoendeshwa na Generation Unlimited, ambayo ilianzishwa na UNICEF, Microsoft, IKEA na wadau wengine ili kukuza ubunifu kama huu.

Chelsea Johannes (kulia) akifafanua jinsi chombo cha choo chao cha kibunifu cha Saniwise kinavyofanya kazi.
© UNICEF/Paul Kidero
Chelsea Johannes (kulia) akifafanua jinsi chombo cha choo chao cha kibunifu cha Saniwise kinavyofanya kazi.

 Choo rafiki

Kikiwa kimetengenezwa kwa nyenzo zilizokwisha tumika hapo awali, pamoja na taka za plastiki, mfano huo wa choo kinachojali mazingira unatumia teknolojia ya kukausha choo kikavu. Baada ya kuzuru choo, askari mweusi anarusha mabuu ya kinyesi cha binadamu kuwa samadi.

"Huyu ni askari mweusi anayeruka mabuu," alisema, akionesha vijidudu kadhaa vyeupe kwenye sakafu ya choo. "Wanayeyusha taka. Unaweza kuona kwamba tayari inaonekana zaidi kama udongo. Katika muda wa siku nne, itakuwa tayari kuuzwa kama samadi."

 

‘Vijana wanajisaidia wenyewe’

Saniwise Technologies pia inauza bidhaa hizo kwa wakulima wa ndani, kama John Ochieng mwenye umri wa miaka 77.

Asubuhi yenye joto na unyevunyevu kwenye shamba la Bw. Ochieng, anatembea mashambani miguu peku. Njiani, anakusanya mfuko wa samadi kutoka kwa Bi Johannes na wenzake, baada ya kukutana nao kwenye rasi iliyo karibu.

“Nilikuwa na hamu ya kujua kuhusu choo walichokuwa wamejenga,” alisema. “Waliniambia kuwa kinatengeneza samadi na chakula cha kuku, kwa hivyo nilinunua sampuli kutoka kwao.”

Mbolea tayari kusaidia shamba lake.

“Ninapenda bidhaa zake,” alisema. "Mbolea husaidia mimea yangu kuwa kijani kibichi na kuzaa matunda. Nilipowapa kuku wangu chakula, walifurahia. Ni vizuri kuona vijana wakijisaidia wenyewe.”

Ili kufahamu zaidi jinsi Umoja wa Mataifra unavyosaidia kuharakisha maendeleo katika kuboresha maji safi na usafi wa mazingira duniani kote bofya hapa.