Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maji ni uhai, maji ni chakula usimwache yeyote nyuma katika hili: FAO

Wanawake wanachimba mabwawa ya katikati ya mwezi ili kuokoa maji nchini Niger.
©FAO/ Giulio Napolitano
Wanawake wanachimba mabwawa ya katikati ya mwezi ili kuokoa maji nchini Niger.

Maji ni uhai, maji ni chakula usimwache yeyote nyuma katika hili: FAO

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Leo ni siku ya chakula duniani na maadhimisho ya mwaka huu kwa mujibu wa shirika na chakula na kilimo FAO yanasherehekea moja ya rasilimali muhimu zaidi kwa maisha ya binadamu ambayo ni maji, kwani yanachukua asilimia 50 ya uso wa dunia, yanazalisha chakula na kuwezesha watu kuishi.

Maudhui ya siku ya mwaka huu ni “Maji ni uhai, maji ni chakula, usimwache yeyote nyuma”.

Pamoja na kwamba maji ndio kila kitu FAO imekumbusha kwamba rasilimali hiyo haidumu milele na dunia inahitaji kuacha kuichukulia kama mazoea kwani chakula kinacholiwa duniani na jinsi kinavyozalishwa vinaathiri rasilimali ya maji.

Hivyo shirika hilo limesisitiza kwamba dunia “Kwa pamoja tunaweza kuchukua hatua kwa ajili ya chakula na kuwa mabadiliko yanayohitajika, kwani maji ni msingi kwa ajili ya maisha na chakula.”

Akisisitiza umuhimu huo mkurugenzi mkuu wa FAO Qu Dongyu (TAMKA KYU DONGYU) amesema, “Mgogoro wa madadiliko ya tabianchi, ongezoko la idadi ya watu, ukuaji wa miji, maendeleo ya viwanda na maendeleo ya kiuchumi na kijamii vinaongeza shinikizo katik rasilimali ya maji.”

Na kuongeza kuwa theluthi moja ya watu wote duniani wanaishi bila rasilimali hiyo muhimu hivyo changamoto hizo zinaleta athari kubwa kwa uhakika wa chakula  na ametoa wito wa kugeukia sayansi, ubunifu na teknolojia kuzitatua,

“Lazima tukumbatie uwezo wa sayansi, ubunifu, takwimu na teknolojia kuzalisha zaidi kwa kutumia maji kidogo ili kufanya kila tone la maji kuwa na maana. Sote tunapswa kutumia na kudhibiti maji kwa ufanisi.”

Ili kuendeleza azma hiyo ametaka sekta ya kilimo inayotumia asilimia 70 ya maji duniani kufanya mabadiliko ya mifumo yake ya chakula na ndio maana leo mjini Roma Italia FAO limenaza kongamano la siku nne litakalokamilika 20 Oktaba kujadili umuhimu wa sayansi, uvumbuzi na teknolojia katika kubadili mifumo ya chakula kuwa sehemu ya suluhu ya mabadiliko ya tabianchi.

Ismahane Elouafi ni mkuu wa kitengo cha sayansi ya chakula na kilimo wa FAO anasema,“Kuanzia uvumbuzi wa teknolojia hadi uvumbuzi wa kifedha, uvumbuzi wa kitaasisi, uvumbuzi wa sera, ni katika wigo mzima wa uvumbuzi, na tunatumai kwamba mjadala kati ya wadau tofauti utaleta matokeo, je tunajua nini  hadi sasa, tunaweza kuongeza nini kwa sasa na ni wapi tunapaswa kuwekeza katika siku za usoni ili kuwa na msingi bora wa sayansi na ushahidi kwa ajili ya utungaji sera na kwa ajili ya mabadiliko ya mifumo ya kilimo ya chakula.”

FAO inasema kampeni ya siku ya chakula mwaka huu ni kuelimisha dunia kuhusu umuhimu wa kutumia maji kwa ufanisi kwa sababu rasilimali hiyo iko katika tishio kubwa na huu ni wakati wa kufanyakazi pamoja na kujenga mustakbali bora, na endelevu kwa wote.