Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kwa kifo cha Thomas Buergentha tumepoteza mtetezi wa haki za binadamu - Volker Türk 

Thomas Buergenthal, mnusurika wa mauaji dhidi ya wayahudi, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki na Profesa katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha George Washington.
UN Photo/Manuel Elías
Thomas Buergenthal, mnusurika wa mauaji dhidi ya wayahudi, Jaji mstaafu wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki na Profesa katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha George Washington.

Kwa kifo cha Thomas Buergentha tumepoteza mtetezi wa haki za binadamu - Volker Türk 

Masuala ya UM

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk ameeleza  kuwa kufariki dunia kwa Thomas Buergentha dunia imepoteza mtu mashuhuri wa utetezi wa haki za binadamu, “Muda kamili wa maisha ya Thomas Buergenthal uliakisi na kutufundisha uwezo wa kudumu wa haki za binadamu.” 

Thomas Buergenthal, mwathiriwa wa Auschwitz aliyekua na hata kufikia kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) amefariki akiwa na umri wa miaka 89 tarehe 29 Mei, 2023.  

Bwana Türk akieleza kuhusu maisha ya Thomas Buergentha anasema miaka yake ya kwanza aliishi katika hofu isiyomithilika. “Akiwa mtoto, aliteseka kunyimwa kabisa utu wa kibinadamu katika kambi za mateso za Auschwitz na Sachsenhausen. Akiwa na alama ya kutofutika kwa kunyimwa haki za binadamu kwa Unazi, alinyanyuka - kupitia uwezo wa akili yake, kiu yake ya haki, na imani yake katika uwezo wa ubinadamu kustawi chini ya utawala wa sheria - hadi nyadhifa za juu zaidi za uongozi na akajitahidi kuepusha marudio ya vitisho hivyo vya kutisha.” 

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu anaendelea kueleza kuwa hayati Thomas Buergentha akiwa Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na Mjumbe wa Kamati ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, kama Rais wa Mahakama ya Haki za Kibinadamu ya Amerika, na katika majukumu yake mengine, alikuwa mtetezi wa ulinzi madhubuti wa haki za binadamu na kwa ajili ya kuundwa kwa taasisi madhubuti za kuzitetea na kuzitunza. 

Bwana Türk ametuma salamu za rambirambi “ziende kwa familia ya Thomas Buergentha “na wale wote aliowagusa kupitia maisha ya nguvu na ushawishi wa ajabu.”