Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutokana na madeni ya nje na mfumuko wa bei, nchi zinazoendelea zitapoteza dola bilioni 800: UNCTAD

Gharama kubwa ya chakula inaziathiri nchi zinazoendelea
UN Women/Ryan Brown
Gharama kubwa ya chakula inaziathiri nchi zinazoendelea

Kutokana na madeni ya nje na mfumuko wa bei, nchi zinazoendelea zitapoteza dola bilioni 800: UNCTAD

Ukuaji wa Kiuchumi

Huku kukiwa na msukosuko wa kifedha na kudorora kwa uchumi wa dunia, nchi zinazoendelea zinakabiliwa na miaka mingi ya changamoto za kiuchumi. Hii imeelezwa katika ripoti mpya ya kamati ya Umoja wa Mataifa ya Biashara na Maendeleo (UNCTAD), iliyochapishwa leo.

Wataalamu wanasisitiza kuwa wastani wa viwango vya ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka ni vya chini kuliko kabla ya janga la coronavirus">COVID-19 na hata mdororo wa kiuchumi wa kimataifa.

Kulingana na makadirio ya hivi karibuni ya UNCTAD, uchumi wa dunia utakua kwa asilimia 2.3 mwaka huu wa 2023.

Kupoteza mapato, kuongezeka kwa madeni na ukosefu wa usawa

Wanafunzi nchini Tanzania wakiwa wamebeba  mabango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu - SDGs
UN News
Wanafunzi nchini Tanzania wakiwa wamebeba mabango ya Malengo ya Maendeleo Endelevu - SDGs

Wanauchumi wanaonya kuwa mfumuko wa juu wa bei na viwango vya juu vya riba vitapunguza zaidi ya dola bilioni 800 katika mapato kutoka kwenye nchi zinazoendelea katika miaka ijayo.

Mataifa haya pia yanakabiliwa na kuongezeka kwa madeni la nje, kupanda kwa bei ya vyakula kutokana na mfumuko wa bei, na ukosefu wa kuungwa mkono kimataifa.

Kwa mujibu wa UNCTAD, nchi 81 zinazoendelea ukiondoa China zilipoteza dola bilioni 241 katika akiba zao za kimataifa mwaka 2022, huku nyingi zikipoteza haki ya kuchua akiba zao za ziada (SDR).

Wakati huo huo, ripoti inasema gharama ya kukopa kwa masoko 68 yanayoibukia iliongezeka kutoka asilimia 5.3 hadi asilimia 8.5 na UNCTAD inatarajia kutakuwa na kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa wadai wa nje kwa nchi zinazoendelea.

Katika ripoti hiyo wataalamu wanasisitiza kuwa deni kubwa litasababisha changamoto za maendeleo na hata kukosekana kwa usawa.

Nchi nyingi zitalipa wakopeshaji zaidi ya walivyopokea katika mikopo mipya, na hivyo kupunguza matumizi ya kijamii kama matokeo ya madeni hayo.

Ripoti hiyo ya UNCTAD inabainisha kuwa leo hii idadi ya nchi zinazotumia fecha zaidi kulipa deni la nje kuliko huduma za afya imefikia 62 ikilinganishwa na nchi 34 miaka kumi iliyopita.

Mtoa huduma za Afya kitengo cha Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kata ya Mkambalani Rebeca Wami akizungumza na mama ambaye amehudhuria mafunzo wakati wa wiki ya unyonyeshaji.
Hamad Rashid
Mtoa huduma za Afya kitengo cha Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kata ya Mkambalani Rebeca Wami akizungumza na mama ambaye amehudhuria mafunzo wakati wa wiki ya unyonyeshaji.

Jinsi ya kusaidia nchi zinazoendelea

Ili kusaidia nchi zinazoendelea kuondokana na matatizo ya kiuchumi, ni muhimu kuimarisha ajenda ya kimataifa ya kifedha, kwa kuweka msisitizo maalum wa kuzingatia marekebisho ya muundo wa madeni, inasisitiza ripoti ya UNCTAD.

Wataalamu, hasa, wanatoa wito wa kuundwa kwa utaratibu wa utatuzi wa kimataifa wa madeni, orodha ya takwimu iliyothibitishwa juu ya miamala ya madeni ya wadai na wakopaji au wadaiwa, pamoja na kuboresha uchambuzi wa masharti ya madeni ambayo yanazingatia mahitaji ya ufadhili wa maendeleo na kupambana na mabadiliko yatabianchi.

Mikutano ya sasa yashirika la fecha duniani  IMF na Benki ya Dunia inatoa fursa ya kuimarisha fedha za maendeleo na kushughulikia changamoto zinazokabili nchi zinazohitaji ukwasi zaidi.

Kutolewa kwa idhini mpya ya kuchukua akiba au SDR yenye thamani ya angalau dola bilioni 650 kunaweza kuwa hatua ya kwanza katika kupunguza mzigo wa madeni unaozuia maendeleo ya nchi, kulingana na UNCTAD.

Wafanyakazi wa Green Care nchini Rwanda wakiwa kwenye dampo. Kampuni hii imejikita katika udhibiti wa taka na kutengeneza mboji au samadi.
UN/ Flora Nducha
Wafanyakazi wa Green Care nchini Rwanda wakiwa kwenye dampo. Kampuni hii imejikita katika udhibiti wa taka na kutengeneza mboji au samadi.

Mpango wa UN na mageuzi ya usanifu wa fedha duniani

Mwezi Februari mwaka huu, mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, aliwasilisha mpango wake wa kuchochea utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Mpango huo unapendekeza mageuzi ya usanifu wa fedha duniani na kutoa uwekezaji mkubwa katika nishati mbadala, ulinzi wa hifadhi ya jamii kwa wote, uundaji wa nafasi za ajira zenye staha, huduma za afya, na elimu bora.

Katibu Mkuu huyo alisema kuwa kila mmoja atafaidika na utekelezaji wa mpango huo, lakini ari ya kisiasa ya viongozi wa dunia inahitajika ili kuufanikisha. Kwa mujibu wske, ubinadamu lazima ukubali mkataba wa Bretton Woods wa 2.0.

Kumbuka kwamba kufuatia matokeo ya mkutano wa Bretton Woods mwaka wa 1944, mfumo wa kimataifa wa kuandaa mahusiano ya kifedha na makazi ya biashara ulianzishwa.

"Bretton Wood 2.0 inahitajika ili, tunapoelekea kutokuwa na uhakika, tunaweza kukidhi mahitaji yaliyowekwa katika hati asili, na pia kuuandaa ulimwengu na wakaazi wake walio hatarini zaidi kwa mustakabali usio na uhakika," amesema Katibu Mkuu alisema.