Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vifo vya raia kutokana na mlipuko wa lori la gesi Afrika Kusini vimenishtua: Guterres 

Katibu Mkuu António Guterres akihutubia mjada wa wazi wa Baraza la Usalama kuhusu ujunzi wa amani na amani endelevu
UN Photo/Eskinder Debebe
Katibu Mkuu António Guterres akihutubia mjada wa wazi wa Baraza la Usalama kuhusu ujunzi wa amani na amani endelevu

Vifo vya raia kutokana na mlipuko wa lori la gesi Afrika Kusini vimenishtua: Guterres 

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema amesikitishwa sana na vifo vya makumi ya raia kutokana na mlipuko wa lori la gesi ulilotokea Boksburg,nchini Afrika Kusini. 

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na msemaji wake mjini New York Marekani Antonio Guterres anatoa pole kwa familia za waliopoteza maisha kutokana na mlipuko huo na kwa wananchi na Serikali ya Afrika Kusini.  

Katibu Mkuu pia anawatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa na ujenzi wa haraka wa miundombinu ya afya iliyoharibika. 

Kwa mujibu wa duru za habari jumla ya watu 34 wamekufa hadi sasa kutokana na mlipuko wa huo wa Boksburg, mkoa wa Gautenguliotokea katika, siku ya mkesha wa Krismasi. 

Imeelezwa kuwa lori lililokuwa limebeba gesi ya petroli lilikwama chini ya daraja la chini huko Boksburg, na mlipuko ulitokea gari hilo liliposhika moto kwa sababu ya msuguano. 

Miongoni mwa waliofariki dunia 11 ni wahudumu wa afya wa hospitali ya Tambo Memorial, takribani mita 100 kutoka eneo la mlipuko, huku wengine 23 wakiwa ni wananchi, kwa mujibu wa waziri wa afya wa nchi hiyo Joe Phaahla, ambaye alisema katika ibada hiyo ya kumbukumbu ya kusaidia familia kukabiliana na athari walioipata.