Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Operesheni za ulinzi wa amani za UN atembelea MINUSCA

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix akiwa ziarani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR
Picha : MINUSCA / Leonel GROTHE
Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix akiwa ziarani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR

Mkuu wa Operesheni za ulinzi wa amani za UN atembelea MINUSCA

Amani na Usalama

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix amekamilisha ziara yake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambapo alikutana na walinda amani na kufanya kufanya mikutano na viongozi wa kijeshi.

Nisalamu za kijeshi…… pamoja na gwaride maalum…… ikiwa ni kumkaribisha Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean-Pierre Lacroix nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR.

Katika ziara hiyo Bwana Lacroix ameambatana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini CAR, Valentine Rugwabiza, ambaye pia ni Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani CAR, MINUSCA.

Bwana Lacroix amesema kilichompeleka nchini humo ni kukutana na walinda amani, anasema …. “Nimekuja kuona wenzetu wapo mashinani wanavyofanya kazi, kuona maendeleo yaliyofikiwa katika kuboresha kambi, kujenga kambi mpya, kuhakikisha wafanyakazi wetu wanaume na wanawake wanakuwa na hali bora ya maisha, na pia kukutana na kikosi cha Ureno na Bhutan na kuwashukuru kwa kazi yao, kuwapongeza kwa yote wanayofanya, na kuwatakia mafanikio mema na, mwisho wa mwaka, wenye kheri na kuwaombe mema katika mwaka ujao, kwao na familia zao.”

Maafisa wengine walioambatana na Lacroix ni Jenerali Birame Diop, Jenerali Daniel Sidiki Traore na naibu wake Jenerali Pedro Miguel Alves Gonçalves Soares, pamoja na Kamanda wa Kikosi Jumuishi cha Bangui, Brigedia Jenerali Alognime Takougnadi.