Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashujaa watanzania wawili miongoni mwa waliotunukiwa medali ya Dag Hammarskjold

Brigedia Jenerali George M. Itang'are, Mwambata wa Kijeshi Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (katikati) akiwa ameshikilia moja ya nishani ya Dag Hammarskjöld ambayo walitunukiwa walinda amani wawili wa Tanzania w
Ofisi ya Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York, Marekani.
Brigedia Jenerali George M. Itang'are, Mwambata wa Kijeshi Ubalozi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa (katikati) akiwa ameshikilia moja ya nishani ya Dag Hammarskjöld ambayo walitunukiwa walinda amani wawili wa Tanzania waliouawa mwaka 2021 wakati wa utumishi wao chini MONUSCO nchini DRC.

Mashujaa watanzania wawili miongoni mwa waliotunukiwa medali ya Dag Hammarskjold

Amani na Usalama

Kuelekea siku ya kimataifa ya walinda amani ambayo itaadhimishwa Jumapili hii tarehe 29 Mei, Umoja wa Mataifa umetoa medali kuwatambua na kuwaenzi walinda amani majasiri. Miongoni mwa medali zilizotolewa ni ya Dag Hammarskjoldna kati ya waliotunukiwa ni askari wawili wa Tanzania waliouawa mwaka 2021 wakiwa katika majukumu ya ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.

Majina ya walinda amani Marehemu Luteni Kanali Christopher Edward Kavalambi na Marehemu Private Daudi Mbwana Ally yakitajwa mbele ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ili kutambuliwa kuwa wametunukiwa medali ya Dag Hammarskjold. 

Katika hafla iliofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo askari hawa marehemu wametambuliwa ujasiri wao kwani walijitolea maisha yao mwaka jana 2021 wakilinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo chini ya mwavuli wa ujumbe wa Umoja huo wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO

Kwa niaba ya Balozi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Profesa Kennedy Gastorn, aliyepokea medali hizo za Tanzania, ni Mwambata wa kijeshi katika ofisi ya Balozi wa kudumu wa Tanzania katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, jijini New York Marekani, Brigedia Jenerali George Itang’are, anatuma ujumbe wa pole kwa familia, ndugu jamaa na marafiki akisema, “kwa niaba ya mheshimiwa Balozi, ninapenda kuchukua fursa hii kufikisha salamu kwa familia za marehemu kwa kuondokewa na wapendwa. Umoja wa Mataifa na Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, pamoja na jumuiya ya kimataifa zinatambua mchango wao wakiwa wanahudumu katika ulinzi wa amani. Mwenyezi Mungu azilaze roho za wapendwa wetu mahali pena peponi.” 

Mashujaa watanzania wawili miongoni mwa waliotunukiwa medali ya Dag Hammarskjold

Medali ya Dag Hammarskjöld ni tuzo ya baada ya kifo inayotolewa na Umoja wa Mataifa kwa wanajeshi, polisi, au raia wanaopoteza maisha wakati wakihudumu katika operesheni ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa. Medali hiyo imepewa jina la Dag Hammarskjöld, aliyekuwa Katibu Mkuu wa pili wa Umoja wa Mataifa, ambaye alifariki Septemba mwaka 1961 kwa ajali ya ndege katika eneo ambalo hivi sasa ni nchi ya Zambia.