Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari ya COVID-19 kwenye utalii zinaweza kusababisha pigo la dola trilioni 4 kwa uchumi wa dunia: Ripoti ya UN

Mlima Kilimanjaro ulioko Tanzania
World Bank/Curt Carnemark
Mlima Kilimanjaro ulioko Tanzania

Athari ya COVID-19 kwenye utalii zinaweza kusababisha pigo la dola trilioni 4 kwa uchumi wa dunia: Ripoti ya UN

Ukuaji wa Kiuchumi

Athari za janga la corona au COVID-19 katika sekta ya  utalii linaweza kusababisha kupotea kwa zaidi ya dola trilioni 4 kwa uchumi wa dunia, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo kwa pamoja na shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD na shirika la Umoja wa Mataifa la utalii UNWTO. 

Makadirio hayo yametokana na hasara inayosababishwa na athari ya moja kwa moja za janga hilo kwenye utalii na kwenye sekta zinazohusiana, na athari ni mbaya zaidi kuliko ilivyotarajiwa hapo awali. 

Mwezi Julai mwaka jana, UNCTAD ilikadiria kuwa kusimama kwa utalii wa kimataifa kutagharimu uchumi wa dunia kati ya  dola trilioni 1.2 na dola trilioni 3.3. 
Anguko kubwa la kuwasili kwa watalii duniani kote mwaka 2020 kulisababisha hasara ya dola trilioni 2.4,  katika uchumi wa dunia ripoti hiyo imesema, na idadi kama hiyo inatarajiwa mwaka huu kutegemeana na fursa za upatikanaji wa kwa chanjo za coronavirus">COVID-19. 
Mpango wa chanjo ya kimataifa ni muhimu 

"Dunia inahitaji juhudi za kimataifa za chanjo ambazo zitawalinda wafanyikazi, kupunguza athari mbaya za kijamii na kufanya maamuzi ya kimkakati kuhusu utalii, ikizingatia mabadiliko ya muundo," amesema Isabelle Durant, kaimu katibu mkuu wa UNCTAD. 
Naye katibu mkuu wa UNWTO Zurab Pololikashvili ameongeza kuwa "Utalii ni njia ya maisha kwa mamilioni ya watu, na kuendeleza chanjo ili kulinda jamii na kusaidia kurejea kwa usalama katika utalii ni muhimu hasa kwa kupatikana kwa ajira na uzalishaji wa rasilimali zinazohitajika, haswa katika nchi zinazoendelea, ambazo nyingi zinategemea sana utalii wa kimataifa,"  

 


    Nchi zinazoendelea zimeathirika zaidi 

Watalii wa kimataifa walipungua kwa karibu bilioni 1, au asilimia 73, mwaka jana, wakati katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2021 kushuka kulikuwa karibu asilimia 88, imesema ripoti hiyo. 
Nchi zinazoendelea zimebeba mzigo mkubwa wa athari za janga la COVID-19 kwenye utalii, huku kukikadiriwa kupungua kwa watalii wanaowasili kati ya asilimia 60 na asilimia 80. 
Wameumizwa pia na ukosefu wa usawa wa chanjo. Mashirika hayo yamesema "kutolewa kwa mfumo wa chanjo ya COVID-19 kumeongeza pigo la kiuchumi kwa sekta ya utalii katika mataifa haya, kwani wangeweza kuchangia hadi asilimia 60 ya upotezaji wa pato la taifa. 

 

Kusimama kwa utalii kimataifa kumeathiri  uchumi
Source: UNCTAD
Kusimama kwa utalii kimataifa kumeathiri uchumi


  Kuchipuka katikati ya hasara 

Inatarajiwa kwamba utalii utakwamuka haraka katika nchi zilizo na viwango vya juu vya chanjo, kama Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Marekani. 
Lakini, watalii wa kimataifa hawatarudi katika viwango vya kabla ya janga hadi mwaka 2023 au baadaye, kwa sababu ya vizuizi kama vile vya kusafiri, kuzuia virusi kusambaa kwa kasi, imani duni ya wasafiri na mazingira duni ya kiuchumi. 
Wakati kurejea kwa utalii kunatarajiwa katika nusu ya pili ya mwaka huu, ripoti hiyo inatarajia upotevu wa kati ya dola trilioni 1.7 na dola trilioni 2.4 mwaka huu wa  2021, kutokana na uigaji ambao unatenga mipango ya kuchochea utalii na sera kama hizo. 

 

  Kinachowezekana kutokea 

Waandishi wanaelezea hali tatu zinazowezekana kwa sekta ya utalii mwaka huu, na matumaini mabaya zaidi yanaonyesha kupungua kwa asilimia 75 kwa watalii wanaowasili kimataifa.

Hali hii inaona kushuka kwa kiwango cha kupokea watalii duniani kwa karibu thamani ya dola bilioni 950, ambazo zitasababisha hasara katika Pato la taifa ya dola trilioni 2.4 , wakati hali ya pili inaonyesha kupungua kwa asilimia 63 kwa watalii wa kimataifa. 

Ya tatu inazingatia viwango tofauti vya utalii wa ndani na wa kieneo. Inadhani kutakuwa na punguzo la asilimia 75 kwa utalii katika nchi ambazo viwango vya chanjo ni kidogo, na asilimia 37 katika nchi zilizo na viwango vya juu vya chanjo, haswa nchi zilizoendelea na baadhi ya nchi za uchumi mdogo.