Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa IDA wa Benki ya dunia umebadili maisha yangu:Adouia

Makao makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington DC.
World Bank/ Simone D. McCourte
Makao makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington DC.

Mradi wa IDA wa Benki ya dunia umebadili maisha yangu:Adouia

Ukuaji wa Kiuchumi

Kutana na Adouia mama mjasiriamali aliyefaidika na kubadili maisha yake na jamii yake kutokana na mradi wa Benki ya dunia kupitia ufadhili wa jumuiya ya kimataifa ya maendeleo (IDA). 

Adouia anaishi Chad nchi ambayo imeghubikwa na umasikini na vita. Aliolewa akiwa na umri wa miaka 13 tu na sasa ana watoto 8. Kwa msaada wa IDA amepatiwa mafunzo ya ufundi umeme katika moja ya mamia ya miradi inayofadhiliwa na IDA. Mafunzo hayo yamemwezesha kuanzisha biashara ya kufunga paneli za sola kijijini kwake, "Hapo mwanzo nilikuwa namtegemea mume wangu , lakini leo hii kutokana na kazi hii bunifu tunapata faida katika kila paneli tunayofunga, tunaendesha maisha yetu kwa kufunga paneli za sola.”

Fikiria maisha ambayo Adouia sasa anayabadilisha kwa kazi yake, na hii inaanzia nyumbani, mshahara wake Adouia unasaidia kusomesha watoto wake 8, wote wanahitimu elimu yao na wanapata ajira na kuwa kizazi chenye werevu na ubunifu. Na kuweza kufunga paneli zote hizo za sola, Adouia ameamua kutoa mafunzo kwa wanawake wengine kuwa mafundi umeme na wafunga sola kama yeye,“tangu nilipojifunza kufanya kazi hii ya kulipwa , nilitaka dada zangu wafuate mfano wangu, endapo watapata ujuzi wataweza kufanya kazi na kujipatia kipato pia”

Kwa hatua hiyo Adouia analeta mabadiliko katika jamii yake,“familia hazina hofu tena kwa sababu hazilipi bili ya umeme. Punde paneli ya sola inapofungwa umeme ni bure kwa sababu unatoka kwenye jua.

Kazi yake imeleta nuru ya nishati safi na ya gharama nafuu ya umeme wa sola kwa watu wengi ambao hawakuwa nayo. Paneli hizo zitasaidia maduka, viwanda na mashamba kuzalisha zaidi na hivyo kufungua mlango wa masoko mapya na uwezekano mwingine wa mustakabali bora kwa kila mtu.