Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya zahma ya Rohingya lazima itoke Myanmar: UN

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamezuru makazi ya Kutupalong yanayohifadhi wakimbizi wa Rohingya huko Cox's Bazaar nchini Bangladesh
©Caroline Gluck/UNHCRicha na ©Caroline Gluck/UNHCR
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamezuru makazi ya Kutupalong yanayohifadhi wakimbizi wa Rohingya huko Cox's Bazaar nchini Bangladesh

Suluhu ya zahma ya Rohingya lazima itoke Myanmar: UN

Amani na Usalama

Suluhu ya zahma ya Rohingya inayoendelea ni lazima itoke nchini Myanmar, umesema leo Umoja wa Mataifa.

Kauli hiyo imesisitizwa leo na wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa walipozulu makazi ya Kutupalong kuliko ma makambi ya maelfu ya wakimbizi wa Rohingya mjini Cox’s Bazaar nchini Bangladesh.


Wajumbe hao wamekutana na wakimbizi na kusia madhila yanayowasibu na hali ngumu waliyonayo. Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wajumbe hao Balozi Kostavo Meza Quadra wa Peru ambaye nchi yake ndio Rais wa baraza la Usalama mwezi huu amesema “tumekuja hap kufahamu ukubwa wa zahima hii na tumepata picha kamili ya hali iliyopo baada ya kuzungumza na watu na kuzuru kambi”.

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamezuru makazi ya Kutupalong yanayohifadhi  wakimbizi wa Rohingya huko Cox's Bazaar Bangladesh
Picha na ©Caroline Gluck/UNHCR
Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamezuru makazi ya Kutupalong yanayohifadhi wakimbizi wa Rohingya huko Cox's Bazaar Bangladesh


Wajumbe hao wa baraza wameahidi kujaribu kufikia suluhu bora iwezekanavyo baada ya kujadili , wakisisitiza kwamba baraza litaendelea kuupa kipaumbele mgogoro wa Rohingya , lakini suluhu haitoweza kupatikana siku moja.


Kesho Jumatatu wajumbe wa baraza la Usalama watazuru Myanmar kama sehemu ya juhudi za kusaka suluhu ya mzozo huo huku wakisisitiza kwamba suluhu hiyo ni lazima itoke Myanmar.


Wajumbe hao pia wameipongeza serikali na watu wa Bangladesh kwa mchango wao mkubwa kwa wakimbizi wa Rohingya ambao wamekumbana na madhila makubwa yaliyowasababisha laki 7 kufungasha virago na kukimbilia Bangladesh tangu 25 Agosti 2017.


Hii ni ziara ya kwanza ya ujumbe wa baraza la usalama kwenye makambi ya wakimbizi tangu Bangladesh ianze kushuhudia wimbi kubwa la wakimbizi wa Rohingya kufuatia operesheni za usalama zilizoambatana na ghasia kama kujibu mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya vikosi vya usalama.