Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Je bia yaweza kugeuzwa nishati ifikapo 2022?

Je bia yaweza kuwa chanzo kikuu cha nishati mwaka 2022? (Picha:http://bit.ly/2CCqfp7)

Je bia yaweza kugeuzwa nishati ifikapo 2022?

Utafiti mpya wa kisayansi  umebaini mbinu ya kugeuza bia kuwa chanzo cha nishati endelevu kwenye injini badala ya kutumia dizeli. Taarifa kamili na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Utafiti huu umefanywa na wanasayansi kwenye Chuo Kikuu cha Bristol, waliofanyikiwa kugeuza kemikali ya ethanol- kiungo shupavu kinachotumika mno kwenye bia, kuwa butanol kupitia mchakato wa kisayansi unaofanana na michakato ya kutakasa petroli.

Wanasayansi wansema mchakato unaonyesha kuwa bia inaweza kutumika badala ya dizeli  bila marekebisho yoyote kwenye muundo wa injini zilizopo sasa.

Tayari ethanol inatumika kutengeneza vyanzo mbadala na endelevu vya mafuta. Kawaida ethanol huzalishwa kutokana na taka kama vile za misitu, miwa au molasesi.

Profesa Duncan Wass,  kiongozi wa utafiti huo amesema, “moja ya manufaa za mafuta ya butanol, yanaweza kutumiwa kwenye magari ya petroli yaliopo sasa bila marekebisho yoyote au kwa kufanya marekebisho kidogo sana katika muudo wake.

Kwa sasa, mchakato huo waweza kuzalisha mamia ya gramu za butanol kutoka kwenye bia ambazo kwa sasa hazitoshi kujaza tanki la mafuta ya gari.

Hata hivyo, inatabiriwa kuwa mafuta haya yaweza kutumiwa viwandani katika kipindi kisichozidi miaka mitano kutoka sasa na kwamba ifikapo mwaka 2022 butanol inaweza kuwa chanzo kikuu cha usafirishaji.