Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana Somalia badilisheni simulizi potofu kuhusu vijana

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana akihutubia vijana huko Mogadishu, Somalia. Picha: UM

Vijana Somalia badilisheni simulizi potofu kuhusu vijana

Nchini Somalia wiki hii wamezindua sera ya taifa ya vijana ambayo kwayo inazungumzia hatua za kukwamua vijana kuelekea utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Uzinduzi huo umefanyika wakati wa mkutano wa taifa wa vijana kwenye mji mkuu Mogadishu ukihudhuria na viongozi wa kitaifa na kimataifa. Miongoni mwao ni mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu vijana Bi. Jayathma Wickramanayake  ambaye amewasihi vijana sasa kushika usukani ili kubadili simulizi potofu ya kwamba kijana ni lazima atatumbukia kwenye misimamo mikali na kuleta ghasia. Vijana nao wa Somalia hawakuwa nyuma walipaza sauti. Je walisema nini? Fuatana basi na Leah Mushi kwenye makala hii.