Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNWomen yaalika wanaume kuonyesha mshikamano na wanawake

Umoja wa Mataifa waonyesha mshikamano na wanawakae katika harakati za ulinzi wa amani. Picha: UM

UNWomen yaalika wanaume kuonyesha mshikamano na wanawake

Ikiwa leo ni siku ya mshikamano duniani, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UNWomen limetaka wanaume wasisalie kimya wakati huu ambapo vyombo vya habari vimegubikwa na habari za wanawake kukabiliwa na ukatili wa kingono. Patrick Newman na ripoti kamili.

(Taarifa ya Patrick Newman)

UNWomen imesema licha ya habari hizo za ukatili wa kingono dhidi ya wanawake na manyanyaso kughubika vyombo vya habari, wanaume wengi wamejiepusha na mjadala na kusalia kimya.

Kupitia kampeni yake ya #HeForShe inayotaka wanaume kusimama kidete kutetea wanawake, UNWOmen inataka wanaume wavunje ukimya na kujiunga na mjadala huo kupitia mitandao ya kijamii.

Kwa mantiki hiyo kupitia siku hii ya mshikamano, UNWOMEN inataka wanaume warekodi ujumbe wa video ukithibitisha azma na ahadi yao kwa umma ya kutokomeza ukatili wa kingono.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNWOmen Phumzile Mlambo Ngucka amesihi wanaume watakaorekodi ujumeb huo wakaribishe marafiki wengine watatu wa kiume kuungana nao kwenye kampeni na kuwauliza swali je nawe ni balozi wa #HeForShe?

Amesema kwa kufanya hivyo wanaume watakuwa wamebeba jukumu hilo waziwazi badala ya kuchukua hatua kimya kimya kwani haitoshi.