Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muda wa MONUSCO waongezwa hadi 2018, askari wapunguzwa

Muda wa MONUSCO waongezwa hadi 2018, askari wapunguzwa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio linaloongeza muda wa ujumbe wa umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO hadi tarehe 31 mwezi Machi mwakani.

Pamoja na kuongeza muda wa ujumbe huo, azimio hilo limegusia suala nyeti lililokuwa linajadiliwa kuhusu kupunguza idadi ya askari, ambapo sasa imepunguzwa hadi askari 16,215.

Azimio limemtaka Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres kufanya tathmini ya majukumu ya MONUSCO kwa wakati huu kuona iwapo majukumu yote ni muhimu.

Akizungumza baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley amesema hatua ya leo imeweka vigezo vya kupima utendaji na kwamba..

(Sauti ya Nikki Haley)

"Nimeguswa kwamba tumepunguza idadi ya askari lakini tumehakikisha ambako kuna askari, watakuwa na ufanisi, mathalani vikosi maalumu, kuhakikisha uchaguzi unafanyika, watu wako salama, tunaangalia matatizo ya kisiasa yanayotokea nchini humo. Suala kwamba tunashinikiza kuwepo kwa utulivu wa kudumu na utawala bora ni jambo ambalo lazima sote tunapaswa kujivunia.”