Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaongoza katika kulinda haki za wakimbizi wa LGBTI

UNHCR yaongoza katika kulinda haki za wakimbizi wa LGBTI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR limeanzisha mafunzo kwa wafanyakazi wa kibinadamu kwa ajili ya kuwapa stadi za jinsi ya kulinda haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja, na vikundi vingine vidogo kijinsia, LGBTI. Taarifa kamili na Joshua Mmali.

Taarifa ya Joshua

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na UNHCR, watu hawa hukumbwa na changamoto nyingi na vitisho mbalimbali wanapokimbia makwao, ikiwemo ubaguzi, ukatili na wanapata shida ya kueleza mahitaji yao.

Mafunzo hayo yanahusu sheria, mawasiliano, masuala ya afya, jinsi ya kuendesha mahojiano, na kadhalika.

Lengo ni kuhakikishia haki za watu wa LGBTI zinaheshimiwa, kwa mujibu wa Volker Turk, Msaidizi wa Kamishna Mkuu wa UNHCR kwa maswala ya ulinzi, akieleza kwamba licha ya mabadiliko makubwa kuhusu masuala hayo, bado ubaguzi unaendelea.

Mitaala ya mafunzo imeandaliwa kwa uhsirikiano wa UNHCR na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM.