Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya UM dhidi ya utesaji yatoa tahadhari kwa Marekani

Makao Makuu ya UM(picha ya UM)

Kamati ya UM dhidi ya utesaji yatoa tahadhari kwa Marekani

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wa kupinga utesaji wameelezea wasiwasi wao kuhusu masuala mengi yanayohusu utesaji Marekani, yakiwemo kuwaweka watu rumande, ukatili wa kingono magerezani na wa wahamiaji haramu, nusura waitangaze Marekani kama nchi inayokiuka sheria za haki za binadamu.

Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu utesaji pia ilidai kuwepo ukiukaji wa haki za binadamu Ukraine, Venezuela na Australia, wakati wachunguzi wake wakikamilisha kikao chao cha hivi karibuni zaidi leo Ijumaa katika Baraza la Haki za Binadamu, mjini Geneva.

Alipoulizwa ikiwa Marekani ilikiuka Mkataba wa haki za binadamu kwa kuendelea kuwazuilia wafungwa Guantanamo Bay, Cuba bila mashtaka, mtaalam maalum Alessio Bruni amesema ni suala linalozua maswali:

“Bila shaka naweza kusema ni suala lisiloweza kuhakikiwa kwa urahisi, kwa sababu, kama unavyojua, kituo hiki cha rumande kimewekwa kwa aina ya wafungwa ambao hawajaainishwa vyema, na wengine wao wameainishwa. Kama vile, je ni maadui wa kivita, na wanaweza kushtakiwa chini ya sheria ya vita?”

Bwana Bruni ameongeza kuwa utesaji popote pale ambapo Marekani ina mamlaka yake hauwezi kukubalika.

Kitu kimoja ni lazima kiwe dhahiri: kuwa kufasiriwa kwa mkataba kupo mikononi mwa serikali ya Marekani. Kwamba kupigwa marufuku utesaji ni halali kwa wafungwa wowote wale, wakiwemo wale wa Guantanamo na vituo vingine vya kifungo. Ni halali popote pale, kwa yeyeote, na bila shaka ukiukaji wa vipingele hivi ni ukiukaji wa sheria.”

Amesema utesaji ni moja tu ya vitu vingi ambavyo vinapaswa kubadilishwa na serikali ya Marekani.