Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban alaani mashambulizi ya Boko Haram kaskazini mwa Nigeria

IRIN/Aminu Abubakar(UN News Centre)
Uhalifu uliofanywa na kikundi cha Boko Haram mjini Kano, Nigeria.

Ban alaani mashambulizi ya Boko Haram kaskazini mwa Nigeria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amelaani vikali mashambulizi ya kutisha yanayoendelea kutekelezwa na kundi la Boko Haram dhidi ya raia kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Ban amesema mashambulizi kama hayo yamefanywa kuwa tukio la kila siku, kama ilivyodhihirika mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya vijiji na makanisa karibu na Chibok, ambako Boko Haram waliwateka wasichana zaidi ya 200.

Katibu Mkuu amerejelea kusema kuwa Umoja wa Mataifa u tayari kuisaidia Nigeria wakati inapoitikia tatizo hilo katika njia inayoendana na wajibu wake wa kimataifa wa haki za binadamu. Ban amepeleka ujumbe wa mshikamano na pole kwa wahanga wa ukatili huo, na watu wa Nigeria.