Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya Wakimbizi wa DRC wamiminika Uganda

Maelfu ya Wakimbizi wa DRC wamiminika Uganda

 Zaidi ya wakimbizi Elfu Nane wa  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Gongo (DRC) wameingia  wilaya ya Kisoro nchini Uganda tangu Jumatatu kufuatia mapigano katika Jimbo la Kivu ya Kaskazini. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM, Uganda ametuma ripoti hii.

(Taarifa ya John Kibego)

Kufuatia mashambulio mapya ya jeshi la serikali yaKinshasalikisaidiwa na jeshi la kujibu mashambulio la Umoja wa Mataifa dhidi ya waasi wa M23 maelfu wamekimbilia hapaUganda. Mapigano hayo yasiyotarajuiwa yameshuhudiwa wakati mipango ya mazungumzo ya amani kati ya DRC na M23 mjiniKampala–Ugandainaendelea.

Tayari Shrika la Umoja wa Matifa Kuhudumia wakimbizi la (UNHCR), limesafirisha wikimbizi 3410 kutoka mpakani hadi mjini Kisoro, kama anavyoeleza Lucy Beck, msemaji wa UNHCR kusini magharibi mwa Uganda.

(Sauti ya Lucy Beck)

Beck amesema wanapanga kuwasafirisha wakimbizi hao hadi kwenye kambi ya wakimbizi ya Rwamwanja wilayani Kamwege ambako tayari kuna wakimbizi 50,000 waliotoroka fujo ya M23 kuanzia mwaka jana.

Wakimbizi wamekuwa wakijitokeza barabarani na vichakani kutoka nchi hiyo yenye madini mengi na makundi mengi ya wanamgambo.

Siku ya Jumatatu wiki hii, zaidi ya wakimbizi 3,000 waliotoroka ukatili wa kundi la M18 walipokewa katika wiaya ya Koboko na mipango ya