Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulowezi wa Israeli ni ishara ya ukosefu wa haki kwa Wapalestina: Ripoti

Ulowezi wa Israeli ni ishara ya ukosefu wa haki kwa Wapalestina: Ripoti

Ripoti mpya ya ujumbe wa kimataifa wa kuhakiki hali katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa imedhihirisha jinsi ulowezi wa Waisraeli unavyoathiri haki za Wapalestina.

Ripoti hiyo ambayo imechapishwa leo, inasema kuwa ulowezi huo umechangia ukiukaji wa haki za Wapalestina kwa njia nyingi.

Ripoti inasema kuwa ukiukaji huo una uhusiano wa moja kwa moja, na unaonyesha mwenendo wa kubana haki ya kujitawala na ubaguzi wa kila siku dhidi ya Wapalestina.

(AUDIO)