Mzozo wa Mashariki ya Kati ni jinamizi kwa wanawake na wasichana: UN Women
Mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati baina ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas na Israeli, kwa siku 18 sasa umesababisha jinamizi kubwa kwa maelfu ya wanawake na wasichana limesema shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na masuala ya wanawake UN Women.