Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Hayat, mkulima na mfugaji akiwa na mbuzi wake huko shambani mwake Badham nchini Somalia.
FAO/Arete/Isak Amin.

Ufugaji endelevu unaonufaisha jamii bila kuharibu mazingira wamulikwa huko Roma, Italia

Mkutano wa kwanza kabisa wa kimataifa kuhusu marekebisho ya mfumo wa ufugaji wa Wanyama umeanza hii leo kwenye makao makuu ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO lengo likiwa ni kusaka mbinu za kuwezesha ufugaji huo uwe na mnepo zaidi, usiharibu mazingira na uchangie katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii, halikadhalika sayari yenye afya.

Sauti
3'5"
Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyoko jijini Mwanza nchini Tanzania
UN News

Gari tembezi na simu ya kiganjani vyachangia udhibiti wa Kifua Kikuu Tanzania

Wakati dunia ikiweka mikakati ya kutokomeza maambukizi ya Kifua Kikuu, au TB, harakati kutokomeza ugonjwa huo nchini Tanzania zimeanza kuzaa matunda, ambapo tayari hospitali ya Rufaa ya Bugando mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki imeanzisha huduma ya matumizi ya teknolojia ya simu kama njia mojawapo ya sio tu kufuatilia wagonjwa, bali pia kuhakikisha wanatumia dawa zao.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 23 Septemba 2023 New York, Marekani.
UN /Cia Pak

Urusi: Mvutano waendelea duniani kati ya ‘wengi walioamka’, na wachache walio mashakani kupoteza uthabiti wao

Urusi imesema mustakabali wa dunia unaumbwa hivi sasa na mapambano kati ya walio wengi duniani wanaounga mkono mgao wenye haki wa maslahi ya dunia na utofauti wenye ustaarabu ilhali upande mwingine ni wachache wanaotumia mbinu za ukoloni mamboleo kuendeleza utawala wao dhidi ya wengine, utawala ambao wanashuhudia ukiyoyoma mbele ya macho yao.

Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia Demeke Mekonnen Hassen akihutubia mjadala mkuu wa mkutano wa 78 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 23 Septemba 2023
UN /Cia Pak

Ethiopia: Tunakaribisha mazungumzo baina yetu na Sudan na Misri kuhusu Bwawa Kuu la Renaissance

Ethiopia imetumia hotuba yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kueleza kuwa iko tayari kwa na mazungumzo na Sudan na Misri kuhusu ujenzi unaoendelea nchini Ethiopia wa Bwana Kuu la Renaissance, GERD, ujenzi ambao umechochea mvutano baina ya taifa hili la Pembe ya Afrika na nchi mbili hizo kwa kutambua kuwa bwawa hilo linatumia maji ya mto Nile.