Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Watoto wanasubiri kupokea chakula cha lishe bora katika klinki moja huko jiji la Nampo, DPRK
© UNICEF/Olga Basurmanova

Korea Kaskazini semeni ukweli na mtende haki kwa watu waliotoweshwa na kutekwa nyara: Türk

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za binadamu Volker Türk hii leo jijini Geneva nchini Uswisi ametoa ripoti ya kina inayoonesha mateso yanayoendelea ya waathirika wa kutoweshwa na kutekwa nyara nchini Korea Kaskazini na kutaka wale wote wanaohusika wachukuliwe hatua za kisheria na kufikishwa mahakamani ndani ya nchi au mahakama za kimataifa.

Emmanuel Ekiru akiwa darasani akichonga penseli yake. Hii ni baada ya kurejea shuleni kutokana na programu ya mlo shuleni inayoendeshwa na UNICEF na wadau kwani Emmanuel alilazimika kuacha shule kutokana na ukame unaokumba kaunti ya Turkana nchini Kenya.
UNICEF VIDEO

Shule zaidi ya 100 zaathirika na ukame Turkana, UNICEF yahaha kusadia watoto kusalia shuleni

Ukame unaoendelea Pembe ya Afrika umeathiri shule zaidi ya 100 katika kaunti ya Turkana Kenya na kusababisha watoto wengi kuacha shule. Sasa shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kenya kwa ushirikiano na mradi wa Educate a child wanaisaidia serikali kusajili watoto shuleni na kuhakikisha waliosajiliwa wanasalia shuleni. 

Sauti
2'41"