Jukwaa la Fez lahitimishwa kwa kuangazia mfano wa Morocco, pia jukumu chanya la Afrika katika nyanja ya kimataifa
Mkutano wa tisa wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Ustaarabu, UNAOC Muungano wa Ustaarabu umehitimisha kazi yake hii leo katika mji wa Fez nchini Morocco, ukisisitiza maadili ya mazungumzo na uvumilivu, lakini pia jukumu la Afrika kama mshiriki chanya katika nyanja ya kimataifa.