Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Naibu Katibu Mkuu wa UN Amina J. Mohammed akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu ajenda ya Wanawake, Amani na Usalama 20-10-2022
UN Photo

Mapigano yanazidi kusigina ajenda ya wanawake, amani na usalama

Mapigano yakiwa  yanaendelea na kurudisha nyuma maendeleo ya haki za wanawake na wasichana duniani, ajenda ya wanawake, amani na usalama bado sana kufanikiwa hivi sasa kuliko wakati wowote ule, imesema ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo wakati ambapo Baraza la Usalama la chombo hicho pia limekutana jijini New York, Marekani katika mjadala wa wazi wa mwaka kuhusu Wanawake,Amani na Usalama: Kuimarisha mnepo na uongozi wa wanawake katika njia ya amani iliyogubikwa na vikundi vilivyojihami.

Wanafunzi wa elimu ya watu wazima katika kituo cha Tumaini kilichoko mtaa wa mabanda wa Kiambiu huko Eastleigh Nairobi, Kenya.
UN/ Thelma Mwadzaya

Elimu ya ngumbaru nchini Kenya yaleta nuru kwa waliodhani hawatojua kusoma na kuandika

Elimu ya watu wazima ni kiungo muhimu kwenye mipango ya maendeleo ya taifa lolote lile. Kutokujua kusoma na kuandika ni kikwazo kikubwa katika harakati za kuimarisha huduma za jamii. Umoja wa mataifa kupitia lengo lake la 4 la maendeleo endelevu,SDGs, unapania kuhakikisha elimu inapatikana kwa wote maishani mwao.Wakaazi wa mitaa ya mabanda huhangaika kupata elimu ukizingatia kuwa juhudi zinaelekezwa zaidi kusaka riziki ya siku na kukidhi mahitaji ya familia.

Walinda amani wa MINUSCA na vikosi vya usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika ulinzi wa amani mjini Bangui, CAR
MINUSCA/Hervé Serefio

Uwezeshaji MINUSCA ni jawabu la ulinzi wa raia CAR- UN

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Valentine Rugwabiza, amesema usaidizi kwa walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo sambamba na juhudi za serikali vimekuwa nguzo ya ulinzi wa raia wakati huu ambapo ukosefu wa usalama unasambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi.