Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Familia iliyotawanywa ikiondoka katika kambi ya ulinzi wa raia ya Umoja wa Mataifa mjini Juba kurejea nyumbani kwao Jonglei Sudan Kusini
UN Photo/Isaac Billy

Mwelekeo wa Mkataba wa Amani Sudan Kusini utupiwe jicho

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuangazia zaidi na kwa mwelekeo wa mkataba wa amani Sudan Kusini pamoja na ongezeko la ghasia miongoni mwa jamii nchini kote Sudan Kusini, wameonya wataalamu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu nchini humo baada ya kuhitimisha ziara yao jijini New York, Marekani ambako wamepata fursa ya kuzungumza na maafisa mbalimbali.

Sauti
2'18"
Naibu Katibu Mkuu Amina Mohammed akihutubia Tamasha la Global Citizen la mwaka 2022 katika Central Park, New York. Tamasha hilo ni tukio la muziki la kila mwaka ambapo mashabiki huchukua hatua za kukomesha umaskini uliokithiri ili kupata kuhudhuria..
UN Photo/Manuel Elías

Raia wa Ulimwengu, mtakuwa mabadiliko tunayoyasubiri? – Naibu Katibu Mkuu UN 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina Mohammed akihutubia umati mkubwa wa watu waliohudhuria ‘Tamasha la Raia wa Ulimwengu’ au Global Citizen Festival, usiku wa kuamkia leo Jumapili katika eneo maarufu kama Central Park jijini New York, Marekani ameuuliza ulimwengu kupitia wakazi wa New York na maelfu wengine waliohudhuria ikiwa wako tayari kuwa mabadiliko chanya ambayo ulimwengu unayasubiri.

Subrahmanyam Jaishankar, Waziri wa Mambo ya Nje wa India, akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 77 cha Baraza Kuu.
UN Photo/Cia Pak

Vita ya Ukraine na Urusi: India iko upande wa amani na itasalia huko

India imesema itaendelezeka ahadi zake za ushirikiano wa pande nyingi, wenye ushahidi uliothibitishwa,  uamuzi wa kusambaza chanjo kwa mataifa zaidi ya 100 duniani, kutoa misaada ya maafa kwa wale walio katika taabu, kushirikiana na nchi nyingine, kwa kuzingatia ukuaji wenye kujali mazingira, muungano bora wa kidijitali na upatikanaji wa huduma ya afya.

Mwanajeshi kutoka Burkina Faso akiwa katika ulinzi kwenye mpaka wa Mali na Niger wakati wa operesheni ya kijeshi dhidi ya washukiwa wa ugaidi.
© Michele Cattani

UN, AU, ECOWAS na G5 Sahel wazindua rasmi Jopo Huru la Usalama na Maendeleo 

Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Sahel uliofanyika Jumamosi hii tarehe 22 Septemba 2022 jijini New York, Marekani pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa (UN), Kamisheni ya Muungano wa Afrika (AU), Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Kundi la nchi Tano za Sahel (G5 Sahel) wamezindua rasmi Jopo Huru la Ngazi ya Juu kushughulikia hali ya Sahel kimataifa.