Wanawake, watoto na wazee ndio walioathirika zaidi na machafuko ya Upper Nile:Nyati
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa shirika la kuratibu misaada ya dharura OCHA nchini Sudan Kusini Bi. Sara Beysolow Nyanti awatembelea waathirika wa machafuko ya hivi karibuni kwenye maeneo ya Adediang na Malakal, katika jimbo la Upper Nile State na kushuhudia madhila yanayowakabili .