Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mwaka 2018, Umoja wa Mataifa uliungana na wengine duniani kote kuzima taa katika Makao yake Makuu na maeneo mengine ili kuadhimisha “saa ya sayari dunia”
UN Photo/Evan Schneider

Jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York kuzima taa zake leo usiku

Leo Jumamosi, tarehe 26 Machi 2022, Umoja wa Mataifa utashiriki tena katika "Saa ya Dunia", mpango wa kimataifa unaounganisha mamia ya mamilioni ya watu binafsi, makampuni, mashirika na serikali duniani kote kuzima taa zao kuanzia saa mbili na nusu usiku (2:30 usiku) hadi Saa tatu na nusu usiku 93:30 usiku) ili kuzingatia masuluhisho ya watu katika kulinda sayari na kujenga mustakabali mzuri na endelevu. 

Mfanyakazi wa maabara akiwa amechukua maji au viambato kutoka katika mimea nchini Ghana ambako asilimia 70 ya wagonjwa hutumia dawa za asili.
WHO/Ernest Ankomah

WHO kuanzisha Kituo cha Kimataifa cha Tiba Asilia

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) na Serikali ya India leo wametia saini makubaliano ya kuanzisha Kituo cha Kimataifa cha Tiba Asilia cha WHO, WHO-GCTM. Kituo hiki cha maarifa cha kimataifa cha tiba asili  kinachofadhiliwa na uwekezaji wa dola milioni 250 kutoka kwa Serikali ya India, kinalenga kutumia uwezo wa dawa asilia kutoka kote ulimwenguni kupitia sayansi na teknolojia ya kisasa ili kuboresha afya ya watu na sayari dunia. 

Mwanamume akiwa na bango linalosema 'bado utumwa upo' akiwa Marekani.
© Unsplash/Hermes Rivera

Tujifunze kwa yaliyopita, tushikamane kutokomeza ubaguzi wa rangi:Guterres 

 Hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kumbukizi ya waathirika na manusura wa biashara ya utumwa katika bahari ya Atlantiki Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema “kuna mengi tunayofahamu kuhusu biashara hiyo na leo ni siku ya kukumbuka uhalifu dhidi ya binadamu, usafirishaji na biashara haramu ya binadamu pamoja na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu usioweza hata kuzungumzika.”