Wanahabari wanapolengwa, jamii kwa ujumla ndiyo inalipia gharama-Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake alioutoa hii leo mjini New York Marekani kuhusu siku ya leo ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji wa sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari, amesema katika siku ya mwaka huu, dunia vikiwemo vyombo vya habari, juu ya changamoto nyingine, vimekabiliwa na changamoto mpya kabisa ambayo ni COVID-19.