Kama nzige hawa hawataisha na mvua ikanyesha japo kiasi, mifugo yetu itakufa- Wafugaji Turkana
Hivi karibuni tulikueleza namna ambavyo nzige wavamizi wa jangwani wanavyotishia ustawi wa wakulima wa Kenya hususani katika eneo la Turkana, lakini kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo la Umoja wa mataifa FAO, nzige hao hawaishii tu katika kilimo bali pia wanatishia jamii ya wafugaji kwani wanakula hadi nyasi na miti ambayo ingekuwa chakula cha kifugo.