Watoto watano wauawa na maroketi Idlib:UNICEF
Wakati mwaka mpya ukianza na vita nchini Syria vikikaribia mwaka wa 10, hali kwa watoto wengi hususan walioko Kaskazini Magharibi mwa nchi ni mbaya sana
Wakati mwaka mpya ukianza na vita nchini Syria vikikaribia mwaka wa 10, hali kwa watoto wengi hususan walioko Kaskazini Magharibi mwa nchi ni mbaya sana
Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limeainisha maeneo 15 ambayo yatahitaji msaada wa dharura na uwekezaji kwa mwaka huu wa 2020.
Leo tarehe pili mwaka 2020, umeshuhudiwa uzinduzi wa mkakati wa Umoja wa Mataifa wa majadiliano makubwa zaidi ya kimataifa kuhusu mstakabali wa dunia. Ni majadiliano makubwa ya pamoja kuhusu jukumu la ushirikiano wa kimataifa katika kujenga mstakabali bora kwa wote. Mpango huo utashuhudia Umoja wa Mataifa ukichochea majadiliano katika mwaka huu mpya wote wa 2020 kwenye mazingira tofauti kote duniani.
Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, doria inayofanywa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi la nchi hiyo, polisi wa Umoja wa Mataifa UNPOL wanaohudumu katika mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo ujulikanao kama MINUSCA inasaidia kuweka utulivu na kukabiliana na uhalifu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amesema ana wasiwasi mkubwa na kumalizika kwa hatua ya usitishaji wa majaribio ya makombora ya nyuklia nchini Jamuhuria ya watu wa Korea au DPRK.
Dunia itahitaji ongezeko la wauguzi na wakunga milioni 9 ili kutimiza ahadi ya kutoa fursa ya huduma za afya kwa wote ifikapo mwaka 2030 limeonya leo shirika la afya ulimwenguni WHO.
Msichana mkimbizi kutoka Damascus Syria ambaye sasa anaishi Uingereza, hivi karibuni alirusha ndege kwa mara ya kwanza akiwa peke yake, ikiwa ni moja ya hatua muhimu katika safari yake ya masomo ambayo yatamfanya kuwa rubani wa kwanza wa kike mkimbizi kutoka Syria.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameungana na dunia kuukaribisha mwaka mpya wa 2020 akiisihi dunia kudumisha amani hasa muongo wa utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu au SDGs ukianza.