Kufa maji kwa baba na mwana toka el salvador hakustahili :UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na kustushwa kuona picha za maiti ya baba na mwana wakimbizi waliokufa maji kwenye ukingo wa Rio Grande
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limesikitishwa na kustushwa kuona picha za maiti ya baba na mwana wakimbizi waliokufa maji kwenye ukingo wa Rio Grande
Leo ni siku ya kimataifa ya mapambano dhidi ya matumizi na usafirishaji haramu wa mihadarati. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni haki kwa ajili ya afya na afya kwa ajili ya haki. Katika mahojiano yangu ya awali kwenye studio zetu za hapa mjini New York, na daktari bingwa wa upasuaji wa ubongo na uti wa mgongo, Dokta Juma Magogo Mzimbiri aliyeko masomoni hapa Marekani amenieleza mihadarati inafanya nini ikiingia katika ubongo wa binadamu.
Kuelekea siku ya biashara ndogo na za kati, SMEs hapo kesho, Umoja wa Mataifa umetaka uwekezaji zaidi kwenye biashara hizo kwa kuwa ndio msingi wa kufanikisha maleng ya maendeleo endelevu, SDGs.
Idadi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Sudan Kusini imepungua, amesema hii leo msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu Andrew Gilmour.
Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu uhuru wa maoni na kujieleza, David Kaye, hii leo ametoa wito wa kuzuiwa haraka kuuzwa, kusafirishwa na kutumiwa kwa teknolojia ya kufuatilia na kuchunguza maisha ya watu hadi pale ambapo mifumo ya udhibiti inayozingatia haki za binadamu itakapokuwepo.
Umri wa mwanamke kuolewa umeongezeka duniani kote na viwango vya uzazi vimeshuka huku wanawake wakizidi kuwa na nguvu kiuchumi, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Umoja wa Mataifa kuhusu mienendo ya maendeleo ya wanawake duniani bila kusahau familia.
Mamilioni ya Wapalestina wanategemea shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kilapestina UNRWA, ili kula , kulala na kuishi na UNRWA haiwezi kukidhi mahitaji hayo endapo nyinyi nchi wanachama na wadau wengine hamtoonyesha ukarimu kwa kunyoosha mkono zaidi kuisaidia
Licha ya kwamba jitihada kubwa zinafanyika barani Afrika kutokomeza njaa tatizo hilo bado limekita mizizi katika maeneo mengi na hatua madhubuti zinapaswa kuchukuliwa haraka ili kuepusha balaa zaidi limesema shirika la chakula na kilimo FAO. Flora Nducha na taarifa zaidi
Viwango vya utapiamlo nchini India ni vya juu kuliko kiwango kinachoweza kuvumilika, imesema ripoti mpya ya uchambuzi wa chakula na uhakika wa chakula iliyotolewa leo kufuatia utafiti wa pamoja kati ay serikali ya India na shirika la mpango wa chakula duniani, WFP.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeibuka na nyaraka yake mpya ambayo inaonesha umuhimu wa samaki wadogo kama vile dagaa katika kufanikisha kutokomeza njaa na kuinua kipato kwa wakazi wa bara la Afrika.