Bila fedha mamilioni ya walio na njaa Yemen watakuwa njia panda:WFP
Wakati mkutano wa kimataifa wa uchangishaji fedha kwa ajili ya Yemen ukifanyika leo mjini Geneva Uswis na kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wa kimataifa na mashirika wahisani, shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limesema linahitaji haraka dola milioni 570 ili kususuru maisha ya mamilioni ya wanaohitaji msaada wa chakula.