UAE mwachieni huru Alia Abdulnour aishi siku zake za mwisho akiwa huru-Wataalamu wa Umoja wa Mataifa.
Watalaamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa hii leo mjini Geneva Uswisi wamezisihi Falme za nchi za Kiarabu UAE kumwachia huru Alia Abdulnour, mwanamke ambaye kwa sasa anashikiliwa katika hospitali ya Tawam licha ya kwamba anasumbuliwa na saratani ya titi.