Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Kituo cha Umoja wa Mataifa cha kulinda Raia, Wau, Sudan Kusini.
UN

Mahakama ya kuhamahama yapeleka haki Malakal, Sudan Kusini.

Kwa zaidi ya kipindi cha siku tatu, mahakama ya kuhamahama inayofadhiliwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, imekuwa katika mji wa Malakal  jimbo la Upper Nile nchini Sudan Kusini ili kushughulikia kesi kadhaa zikiwahusisha watu ambao walitenda makossa makubwa yakiwemo kesi mbili za unyanyasaji wa kingono na moja ya unyanganyi kwa kutumia silaha.

Sauti
2'28"
Jospin (katikati) mkimbizi wa ndani wakiwa kwenye darasa linaloendelshwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa, CAR, MINUSCA.
UNICEF/UN0149422/Sokhin

Elimu  haiwezi kusubiri wapeleka nuru kwa watoto CAR

Serikali ya Jamhuri  ya Afrika ya Kati, CAR kwa ushirikiano na mradi wa Elimu haiwezi kusubiri, ECW,  leo wamezindua mradi wa miaka mitatu wenye lengo la kuboresha elimu nchini humo kama njia mojawapo ya kunasua watoto wa kike na wa kiume kutoka athari za mzozo ulioacha karibu watoto 500,000 bila ya shule.

Wasichana wakijifunza sayansi Vietnam. Kimataifa wasichana wengi wanahudhuria shule kuliko hapo kabla, lakini idadi yao katika masomo ya sayansi au STEM ni ndogo na inaonekana hawa nia ya kuingia katika masomo hayo hasa wanapofikia kuwa vigori
UN Women Viet Nam/Pham Quoc Hung

Ninajiandaa kwa ajili ya nafasi kubwa katika maisha haya.

Kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za utamaduni, takwimu mbalimbali zinaonesha kuwa bado kuna umuhimu wa kuweka mazingira ya kuwahamasisha wasichana kujiunga katika fani za sayansi. Fatima Khamis kutoka Sudan ni mwanamke pekee katika kitengo cha uhandisi wa mitambo ya mawasiliano ya walinda amani walioko chini Jamhuri ya Afrika ya kati.

Sauti
2'