Ziarani Somalia, Di Carlo awahakikishia viongozi ushirikiano wa UN
Mkuu wa Idara ya Siasa kwenye Umoja wa Mataifa Rosemary DiCarlo amewasili nchini Somalia leo ambapo amekaribishwa na rais Mohamed Abdullahi Mohamed na Waziri Mkuu Hassan Ali Khaire, imesema taarifa ya pamoja iliyochapishwa kwenye wavuti wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM.