Zaidi ya wahamiaji 97,000 wavuka Mediteranea mwaka huu pekee kusaka maisha bora Ulaya
Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, limesema idadi ya wahamiaji na wakimbizi walioingia Ulaya kwa njia ya bahari kuanzia Januari mosi hadi tarehe 28 mwezi huu wa Oktoba ni 97,857 ikionyesha kuwa imepungua ikilinganishwa na 147,170 katika kipindi kama hicho mwaka jana.