Nilichoshudia Cox’s Bazar kimenikumbusha wajukuu zangu- Guterres
Kiwango cha machungu waliyopitia warohingya nchini mwao, ukichanganya na madhila ambayo wanapitia hivi sasa huko Cox's Bazar ni kikubwa mno na ni lazima jamii ya kimataifa iongeze msaada wake wakati huu ambapo tayari Bangladesh imefungua mipaka kunusuru warohingya ambao wengi wao ni waislamu.