Mapigano Afghanistan yaengua mamilioni ya watoto shuleni Afghanistan
Mustakhbali wa watoto Afghanistan mashakani kutokana na mapigano
Mustakhbali wa watoto Afghanistan mashakani kutokana na mapigano
Wakati wakimbizi wa Ronhingya kwenye kambi za Cox’s Bazar na jamii zinazowahifadhinchini Bangladesh wakijiweka tayari kwa msimu wa monsoon unaoambatana na upepo mkali na mvua kubwa, shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM, kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh wapo mstari wa mbele kuhakikisha watu hao wanapata msaada wa hali na mali ili kukabiliana na janga hilo
Ulimwengu unahitaji ufumbuzi mbadala dhidi ya matumizi ya vifaa vya plastiki vinavyotumika mara moja na kutupwa.
Hatua za haraka ni lazima zichukuliwe ili kukabiliana na magonjwa sugu pamoja na magonjwa ya akili ambayo yanaongoza kwa kusababisha vifo pamoja na changamoto za kiuchumi na kimaendeleo
Wakati kilimo cha kibiashara kinaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kuchagiza maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, Umoja wa Mataifa unasema hilo linawezekana zaidi iwapo mkulima wa kijijni naye atajengewa uwezo kupitia vyama vya ushirika.
Watu 12 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa baada ya wasafirishaji haramu wa binadamu nchini Libya kuwafyatulia risasi watu 200 waliokuwa wakishikilia mateka wakati walipojaribu kutoroka.
Umoja wa Mataifa umesema walinda amani waliopoteza maisha wakihudumu kwenye maeneo hatarishi zaidi duniani, walijitoa mhanga ili kuhakikisha dunia inakuwa pahala salama zaidi.
Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR linahitaji msaada wa haraka wa dola milioni 116 ili kuendeleza mpango wa kusaidia wakimbizi wa Syria wasiojiweza nchini Jordan.
UNHCR inasema fedha hizo zisipopatikana, italazimika kukata msaada wa fedha kwa wakimbizi wa Syria walioko Jordan ikiwemo walio taabani.