Uzee haukwepeki ni safari ya kila mmoja:UN
Mtaalam wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Georgia kuweka kipaumbele cha mkakati wa kuwajumuisha wazee na pia kuzingatia usawa wa watu hao.
Mtaalam wa kujitegemea wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Georgia kuweka kipaumbele cha mkakati wa kuwajumuisha wazee na pia kuzingatia usawa wa watu hao.
Leo ni siku ya maji duniani ambapo Umoja wa Mataifa unapigia chepuo uhifadhi wa mazingira halisi ya eneo husika kama njia moja ya kukabiliana na uhaba wa maji duniani.
Tangu mwezi disemba mwaka 2013, Sudan K usini imekuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Maelfu ya watu wamekimbilia nchi jirani na wengine wamesaka hifadhi kwenye maeneo mengine ya nchi. Hata hivyo hivi sasa wengine wameamua kurejea na kilio chao sasa ni kwa mwenyezi Mungu.
Vijana wana fursa klubwa ya kuchangia katika kupata suluhu ya changamoto za wakimbizi hususani barani afrika endapo watashirikishwa kikamilifu.
Balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Cate Blanchett ametaka hatua za dharura kulinda na kusaidia wakimbizi wa Rohingya walioko Bangladesh, wakati huu ambapo pepo za monsuni zinatishia usalama wao.
Kuwekeza katika maeneo yenye mazingira bora ya kijani kunaweza kusaidia kubadili miji kuwa endelevu, yenye mnepo, yenye usawa na yenye kupendeza kuishi, limesema leo shirika la chakula na kilimo FAO likiadhimisha siku ya kimataifa ya misitu ambayo kila mwaka huwa Machi 21.
Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limeonya leo kuwa hali ya wafugaji Somalia ni hoi bin taaban kutokana na ukame unaokumba eneo hilo.
Wakati dunia ikiadhimisha siku ya ushairi duniani hii leo, siku iliyotengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwa lengo la kuchagiza usomaji, uandishi, uchapishaji na ufundishaji wa ushairi, mwaka huu imetoa msukomo katika kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.
Eneo la biashara huru limeridhiwa hii leo na hivyo kutoa fursa kwa nchi za Afrika kuimarisha biashara baina yao na hivyo kukuza siyo tu uchumi bali pia maisha ya kijamii ya wakazi wake.
Watu bilioni 1.7 wanaishi vijijini kote duniani huku zaidi ya asilimia 40 ya nguvu kazi yao katika kilimo ni wanawake ambao wakiilisha na kuindeleza jamii lakini wanasalia kuwa ndio masikini wakubwa.