Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Habari Mpya

Mradi wa PACE umepitishwa na Mkutano wa Bali

Wajumbe wa kimataifa waliokutana wiki hii kwenye mji wa Bali, Indonesia kuzingatia Mkataba wa Basel juu ya udhibiti bora wa taka za vifaa na zana za elektroniki wameafikiana kuanzisha mradi mpya utakaojulikana kama mpango wa PACE. Mradi wa PACE unatarajiwa kuandaa mwongozo maalumu wa kiufundi juu ya namna ya kurejeleza matumizi ya zile kompyuta zilizokwishatumika, hasa katika matengenezo madogo madogo na kwenye huduma za vipimo vya kisasa vya kompyuta, ili kutathminia matumizi ya vifaa hivyo vya elektroniki havitochafua mazingira.~

Lampedusa kuwakumbuka wahamiaji waliopotea baharini

Shirika la Kimataifa juu ya Wahamaji (IOM) litakuwa na taadhima maalumu Ijumamosi katika kisiwa cha Lampedusa, Utaliana ambapo kutafunguliwa rasmi mnara wa ukumbusho wa mita tano, wenye umbo la mlango unaokabili bahari inayoelekea Ulaya, uliokusudiwa kuwakumbuka maelfu ya wale wahamiaji waliopoteza maisha baharini pale walipohama makwao kutafuta maisha bora Ulaya. Mnara huo ulifinyangwa na msanii wa Kitaliana Mimmo Paladino. Mradi huu wa kumbukumbu ulijumuisha mchango wa Serikali ya Utaliana, shirika la UM juu ya Wahamiaji (UNHCR), serikali za miji ya Sicily, Puglia na Milan na pia Shirika la IOM na mashirika yasio ya kiserkali ya Kitaliana. ~

Miripuko ya UKIMWI ifasiriwe kihadhi kuwa ni "baa ya ulimwengu", inasema IFRC

Shirika la Kimataifa la Jumuiya za Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) kwenye "Ripoti ya Mwaka ya Maafa Duniani" ilipendekeza janga la UKIMWI ulimwenguni, hususan katika Kusini mwa Afrika, litambuliwe kwa uzito unaolingana sawa na majanga ya mafuriko na njaa. Ripoti ilisisitiza ya kwamba fasiri ya UM juu ya maafa inalingana kikamilifu na athari za maradhi ya UKIMWI duniani.

Haki Zimbabwe lazima itimiziwe waathiriwa wa vurugu la uchaguzi, anasihi Arbour

Louise Arbuor, Kamishna Mkuu wa UM juu ya Haki za Binadamu amenakiliwa akisema kwamba angependa kuona haki inakamilishwa Zimbabwe, mapema iwezekanvyo, dhidi ya wale watu walioshiriki kwenye kampeni za kisiasa, zilizokiuka maadili ya kiutu, na zilizochafua utaratibu wa kidemokrasia nchini humo, kufuatilia duru ya kwanza ya uchaguzi wa taifa mnamo Machi 29 (2008).~

Taka za elektroniki zahatarisha afya ya umma: UNEP

Achim Steiner, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Hifadhi Mazingira (UNEP)ametoa onyo linalohadharisha walimwengu ya kuwa mamilioni ya zile simu za mkononi na kompyuta zinazotupwa ovyo kwenye majaa ya kimataifa, katika sehemu mbalimbali za dunia, huhatarisha afya ya umma kijumla.

Nchi wanachama zahimizwa kuidhinisha mkataba dhidi ya mateso

Tarehe ya leo, Juni 26, inaheshimiwa kuwa Siku ya Kimataifa ya Ushikamano na Waathiriwa wa Mateso, siku ambayo KM aliitumia kutoa mwito unayoyahimiza Mataifa Wanachama wa UM kuidhinisha haraka Mkataba dhidi ya Mateso, na pia kuridhia Itifaki ya Khiyari ya Mkataba huo ambao hujumuisha pendekezo la kuchunguza, bila ya vizuizi, vituo vya kufungia watu vya kitaifa na kimataifa, ili kutathminia utekelezaji wa haki za wafungwa. ~