Njaa inaongezeka Gaza hakuna chakula wala nishati ya kupikia na kukaribisha magonjwa zaidi: WHO
Njaa imeukumba Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia ongezeko la magonjwa hususan miongoni mwa watoto, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na makundi mengine yaliyo hatarini na nishati ya kupikia nayo imeota mbawa.