Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Watoto waliotenganishwa na wazazi wao wakati kijiji chao kiliposhambuliwa mwezi Oktoba wakutanishwa na wazazi wao.
© UNICEF/Benekire

Nilijua watoto wangu wameshafariki dunia sitawaona. Asante UNICEF. Asante CAJED – Mzazi DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kwa kushirikiana na wadau wake kama shirika lisilo la kiserikali la CAJED (CONCERT D’ACTIONS POUR JEUNES ET ENFANTS DÉFAVORISÉS), wanaendelea na huduma kadhaa muhimu za ulinzi kwa watoto ambazo ni pamoja na utambulisho, matunzo na kuwaunganisha watoto na familia zao.  Taarifa ya Anold Kayanda inaeleza zaidi kuhusu tukio la hivi karibuni la watoto kuunganishwa na familia yao.  

Sauti
2'32"
Jeannette Uwimana, mshiriki wa kwanza kiziwi na bubu katika mashindano ya ulimbwende ya Rwanda na ameibuka mshindi katika kipengele cha Mlimbwende na ubunifu wa miradi mwaka 2022.
UNDP Rwanda

Jeanette hakukubali ulemavu alionao kuzima ndoto yake; aibuka mshindi kipengele cha uvumbuzi

Kuelekea siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu duniani kesho tarehe 3 mwezi Desemba, maudhui makuu yakiwa nafasi ya uvumbuzi katika kuchochea dunia yenye fursa za kufikiwa na zenye usawa kwa wote, tunakwenda nchini Rwanda ambako huko mashindano ya ulimbwende kwa mwaka huu wa 2022 yalikuwa ya aina yake kwani kwa mara ya kwanza mshiriki ambaye ni bubu na kiziwi alijumuika na kuibuka mshindi wa kipengele cha uvumbuzi.

Sauti
2'23"
Bi. Salma Mukansanga, Mchechemuzi wa UNICEF kwa kipindi cha miezi 12 ili kusaidia utekelezaji wa Mkakati wa Uchechemuzi chini ya UNICEF Rwanda.
©UNICEF/Steve Nzaramba

Salima Mukansanga - Kama mimi nimefika Kombe la Dunia, hakuna ambako huwezi kufika

Michuano ya fainali za Kombe la Dunia kwa mchezo wa soka kwa wanaume inaendelea nchini Qatar huko Mashariki ya Kati. Mmoja wa watu wanaong’ara katika michuano hii ni Mchechemuzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Rwanda, Salima Mukansanga, ambaye ameweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza mweusi kuwa mwamuzi au refarii katika Kombe la Dunia. Aliingiaje katika tasnia hii ya mpira wa miguu? UNICEF Rwanda ilizungumza naye kabla hajasafiri kwenda Qatar na hapa Anold Kayanda anaeleza kwa lugha ya Kiswahili kilichozungumzwa. 

Sauti
2'39"
Virusi vya ndui ya nyani vinaweza kusambazwa kupitia malengelenge
© Harun Tulunay

Monkeypox au Ndui ya Nyani yabadilishwa jina sasa kutambulika MPOX

Baada ya mfululizo wa mashauriano na wataalamu wa kimataifa, hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO litaanza kutumia jina MPOX badala ya Monkeypox au homa ya Ndui ya Nyani kufuatia mapendekezo ya kubadilishwa kwa jina hilo kwa maelezo ya kwamba lilikuwa linasababisha mambo kadhaa ikiwemo unyanyapaa. 

Sauti
2'24"