Chonde chonde DRC sitisheni uhasama na kuwawajibisha wauaji wa raia:Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amerejea wito wake wa kusitisha uhasama kimataifa na kuyataka makundi yote yenye silaha kuweka silaha hizo chini na kujiunga katika mchakato wa amani, baada ya raia zaidi ya 20 kuuawa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.