Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Watoto hawa katika jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji wanakabiliwa na janga la ukosefu wa chakula, halikadhalika wako hatarini kukumbwa na magonjwa.
WFP/Falume Bachir

Hali bado ni tete kwa watoto Cabo Delgado

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema takribani watoto 250,000 wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia zinazoendelea kwenye jimbo la Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji na sasa wako hatarini kupata magonwa ya kuambukiza kwa kuwa msimu wa mvua unaanza.

Sauti
1'54"
Mtoto mkimbizi kutoka Syria akiwa kwenye makazi ya muda nchini Lebanon.
UNICEF/ Dar Al Mussawir

Majira ya baridi yameanza Lebanon wakimbizi wahaha huku ukata ukizidisha adha:UNHCR 

Maelfu ya wakimbizi nchini Lebanon sasa wanaanza kuhaha kwani majira ya baridi yamewadia na kila mwaka huwapa changamoto kubwa lakini mwaka huu madhila yanatarajiwa kuongezeka kutokana na mgogoro wa kiuchumi na mfumoko wa bei ulioanza Oktoba mwaka 2019 ambao sasa umefikia asilimia 174. Yote haya yanamanisha fedha na msaada wanaopewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR hautokidhi mahitaji.

Sauti
2'26"
Ukosefu wa utaifa ni changamoto
© UNICEF/UNI193657/Esiebo

Usiombe ukutwe na hali ya kukosa utaifa!  

Kutana na Mpho Modise, mama wa watoto wanne ambaye licha ya kuishi nchini Afrika Kusini hana uhakika wa utaifa wake na hivyo anashindwa kupata huduma za msingi kama vile afya na hofu yake kubwa ni kwamba shida inayomkabili yeye ya kukosa utaifa inaweza kuhamia kwa watoto wake labda apate utaifa wa Afrika Kusini.

Sauti
2'21"
Wakimbizi warohingya bado wanaishi wilaya ya Cox's Bazar nchini Bangladesh miaka kadhaa tangu wakimbie nchi yao ya Mynamar
© UNFPA Bangladesh/Carly Learson

WFP imelifungua tena soko la wakulima Cox's Bazar baada ya kulifunga sababu ya COVID-19 

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP wiki hii limelifungua  tena soko kubwa la wakulima kwenye kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh baada ya kulifunga kwa miezi kadhaa kufuatia mlipuko wa janga la corona au COVID-19. Soko hilo ambalo ni sehemu ya mradi wa WFP ni neema sio tu kwa wakimbizi bali pia jamii inayowahifadhi.

Sauti
2'35"