Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari Mpya

Huduma za intaneti nazo zinapatikana sokoni Yambio ambapo vijana wanapata fursa ya kurambaza wavuti mbalimbali ili kupata taarifa
UN /Nektarios Markogiannis

Biashara mtandaoni kiungo muhimu cha kufanikisha SDGs Afrika -UNCTAD

Afrika haitofikia malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs iwapo haitokumbatia fursa ya kuwekeza katika biashara ya mtandao, amesema Katibu Mkuu Mtendaji wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya biashara na maendeleo, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi wakati wiki ya mkutano wa biashara mtandaoni barani Afrika ikifunga pazia leo Jijini Nairobi Kenya.