Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukraine

UNDP inasaidia kutegua mabomu ya ardhini nchini Ukraine.
UNDP in Ukraine/Alexander Ratushnyak

Uondoaji wa mabomu ya kutengwa ardhini Ukraine ni mtihani na hatari kubwa: Paul Heslop

Umoja wa Mataifa umesema Ukraine sasa ni moja ya nchi zilizoathiriwa zaidi na mabomu ya kutegwa ardhini duniani huku ikadiriwa kwamba karibu thuluthi moja ya nchi hiyo imeghubikwa na vita eneo ambalo ukubwa wake ni mara nne na nusu ya nchi ya Uswisi. Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanya kazi na serikali ya Ukraine kwa miaka 30 na umekuwa ukiongoza mpango wa utekelezaji wa uteguaji wa mabomu ya kutegwa ardhini tangu 2016. 

Sauti
2'33"
Olga (kushoto) akiwa na mbwa na mtoto wake, waathirika wa vita inayoendelea nchini Ukraine.
UNHCR Video

Bila UNHCR sijui ningekaa wapi: Olga muathirika wa vita Ukraine

Kutana na Olga mwathirika wa vita inayoendelea nchini Ukraine ambaye baada ya nyumba yake kushambuliwa na kombora mjini Borodyanka alikataa tamaa ya Maisha lakini sasa mradi wa UNHCR wa kukarabati nyumba zilizoharibiwa na vita Ukraine umemfufulia matumaini ya Maisha yeye na mwanaye “Katika maisha mambo hayawezi kuwa mteremko tu, kuna wakati unapitia magumu na ukiwa na uvumilivu utayashinda.

Sauti
3'9"