Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 MEI 2024

08 MEI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika, na wakimbizi wanaorejea nchini Sudan Kusini kutoka Sudan. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni?

  1. Wiki za mvua kubwa na mafuriko huko Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika kumechuochea ukimbizi amapo mamia ya maelfu ya watu wamefurushwa makwao huko Burundi, Kenya, Rwanda, Somalia na Tanzania ambapo Umoja wa Mataifa unasema hadi tarehe 3 mwezi huu wa Mei, jumla ya 637,000 wameathiriwa, 234,000 kati yao hao wamelazimika kukimbia makwao.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao.
  3. Katika makala Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nchini Tanzania, Abeida Rashid Abdallah hivi karibuni akiwa katika safari ya kikazi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani kushiriki vikao vya mkutano wa 68 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW68, alipata nafasi kuzungungumza na Anold Kayanda.
  4. Na mashinani inatupeleka katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri wa Kidemkrasia ya Congo DRC, ambako mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa siku kadhaa sasa zimesababisha maafa, ikiwemo maelfu ya familia kuathirika. 

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'38"