Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

06 MEI 2024

06 MEI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama huko Rafah kusini mwa ukanda wa Gaza, na mafuriko nchini Kenya huku mashirika wakihaha kusaidia waathirika. Makala tunasalia na mada hiyo ya mafuriko Afrika mashariki na mashinani tunakupeleka nchini Sudan, kulikoni? 

  1. Janga la kibinadamu likizidi kushamiri kila uchao huko Ukanda wa Gaza, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaonya kuwa kuzingirwa kijeshi kwa eneo hilo sambamba na operesheni za ardhini za kijeshi huko Rafah kutasababisha janga kubwa kwa watoto 600,000 waliosaka hifadhi kwenye eneo hilo..
  2. Wingu kubwa la mvua likiwa limetanda kwenye mji wa Garsen, ulioko kaunti ya Mto Tana nchini Kenya, Eva Ghamaharo, mama wa watoto watatu anarejea nyumbani akitembea na watoto wake wawili mapacha wenye umri wa miaka mitatu baada ya kununua matumizi ya nyumbani kutoka kioski cha jirani. Watoto hawa wawili mapacha wa kike ni Grace na Jane na wanaonekana na furaha kwani angalau leo mama yao ameweza kuwanunulia kila mmoja pakiti ya maziwa na wanakunywa kwa furaha..
  3. Makala inaangazia madhila ya mafuriko kwa wakimbizi kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katuka ukanda wa Afrika Mashariki.
  4. Na mashinani tutaelekea Darfur nchini Sudan kusikia ni kwa jinsi gani Umoja wa Mataifa umerejesha matumaini kwa waathirika wa vita.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'59"