Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

29 APRILI 2024

29 APRILI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia mzozo na hali ya kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na msaada wa kibinadamu nchini Ethiopia. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Somalia, kulikoni? 

  1. Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya hii leo juu ya idadi kubwa ya watoto ambao wako peke yao Gaza, ama wamepoteza wazazo au kutenganishwa nao pamoja na jamaa wa familia pia wakati huu ambapo hawawezi kuhudhuria masomo na shule nyingi zikigeuka kuwa makazi ya wakimbizi wa ndni.
  2. Nchini Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP na wadau wake waanafanya kazi kwa kushirikiana na jamii kutambua wale wenye uhitaji zaidi wa msaada wa kibinadamu, na wananchi wamepongeza WFP kwa mfumo huu mpya wa kutambua wenye uhitaji zaidi.  
  3. Makala inakwenda nchini Tanzania kumulika ni kwa vipi mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza mitaji, UNCDF uitwao CookFund unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya umesaidia wajasiriamali hasa wanawake kuinua wanawake wenzao kwenye sekta ya matumizi ya nishati jadidifu na hivyo kutekeleza ajenda ya 2030 ya Umoja wa Mataifa ya sio tu kuondokana na umaskini bali pia kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi.
  4. Mashinani ikiwa ni wiki ya chanjo, kniniki tembezi inayofanikishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF imekuwa uti wa mgongo wa mfumo wa afya nchini Somalia na tunakutana na Jamila Moham, Mhudumu wa afya ya jamii katika kijiji cha Dhusamareeb.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu! 

Audio Credit
Leah Mushi
Sauti
11'8"