Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

25 APRILI 2024

25 APRILI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Samante Anne kutoka shirika lisilo la kiserikali nchini Kenya la Mainyoito Pastoralists Intergrated Development Organization (MPIDO) anaeleza namna mabadiliko ya tabianchi yalivyoathiri jamii za watu wa asili nchini mwake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki. 

  1. Leo ni siku ya Malaria duniani ambapo mwaka huu inahamasisha kuongeza mapambano dhidi ya ugonjwa huu ili kuwa na ulimwengu wenye usawa zaidi kwani imebainika kuwa watu wanaoishi katika mazingira magumu ndio wanaoathirika zaidi.
  2. Leo pia ni siku ya kimataifa ya wasichana katika tehama na mwaka huu inasherehekea uongozi ikisisitiza hitaji muhimu la kuwa na mifano thabiti ya wanawake viongozi katika taaluma ya sayansi, teknolojia, uhandishi na hisabati -STEM kwani hali ilivyo sasa kuna wanawake viongozi wachache katika maeneo hayo.  
  3. Na tukisalia na masuala ya wasichana katika tehama Shirika la Umoja Wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limetoa ripoti inayoonya kuwa pamoja na faida za kufundisha na kujifunza kidigitali maendeleo hayo ya kidigitali yanaweza kuwaathiri wasichana kwa kuingilia faragha zao, kuvuruga masomo yao na unyanyasaji mtandaoni.
  4. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu leo ni Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya maneno “Adhimisha na Azimisha.”.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
10'20"